Monday, March 8, 2010
TOTO " NAOMI ANASAKWA NA MWERA!
Mwanamitindo maarufu ulimwenguni,Naomi Campbell,yaelekea akaingia matatani tena kwani hivi sasa polisi wa jijini New York nchini Marekani,wanamsaka!
Naomi,ambaye mwaka jana alitua nchini Tanzania na kushiriki katika onyesho la hisani kwa ajili ya akina mama, safari hii anatafutwa akikabiliwa na shutuma za kumchapa vibao dereva wake huko New York.
Mwanamitindo huyo ambaye inasemekana ni mpenda ugomvi sio mgeni na vyombo vya usalama.Siku za nyuma amekwisha kutwa na hatia ya kumpiga mfanyakazi wake wa ndani jijini New York, kumpa kibano msaidizi wake jijini Toronto na pia kumwangushia kisago polisi ndani ya ndege katika uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London.Katika makosa yote hayo hapo juu,Naomi alikiri makosa yake na alihukumiwa kufanya kazi za kijamii(community services) kwa masaa zaidi ya 200.Kazi kweli kweli.Hivi kwanini kuna baadhi ya watu huwa wanadhani wanayo haki ya kuwaadhibisha watu wengine kiholela tu?Ni matunzo,jamii au?
NB:Hivi unajua Naomi Campbell alipokuwa mdogo alishiriki katika video ya Mfalme wa Reggae,Bob Marley katika wimbo One Love? Mtizame katika video hiyo hapo chini.Alikuwa na umri wa miaka 7 tu na hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa katika spotlight.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment