Wednesday, October 13, 2010

MMMMH!


Na Rhobi Chacha
KABLA ya siku arobaini (40) kutimia tangu kifo cha Mkurugenzi Msaidizi wa Bendi ya Diamond Musica, marehemu Parfect Kagisa ‘P.Diddy’, mchumba wake ambaye ni Mtangazaji wa Kipindi cha B&M kinachorushwa na runinga ya Taifa (TBC1), Maimartha Jesse ‘Mai’ (pichani) anadaiwa kupata bwana mwingine.

Mtoa habari wetu alitupasha kwamba Mai amepata bwana mwingine ambaye amemuwekea mikakati mikali ya kumficha ili asijulikane mbele za watu kwa kuwa ni mapema mno tangu kutokea kufiwa na kipenzi chake P. Diddy.

Pamoja na kuonekana kwamba bwana huyo ni mpya lakini mtoa habari wetu amedai kuwa Mai amekuwa na bwana huyo kwa kipindi kirefu hata kabla ya kifo cha P. Diddy.

Baada ya kupata nyeti hizo, mwandishi wetu alimvutia waya Mai na kumuuliza kuhusiana na suala la yeye kuwa bwana kabla hata ya siku 40 za kifo cha P. Diddy, mtangazaji huyo alishindwa kukanusha habari hiyo.

“Unajua pamoja na P. Diddy kuondoka duniani lakini bado yuko rohoni mwangu, kuhusu suala la kuwa na bwana mimi ni binadamu niliyekamilika, kwanini nikose bwana au unataka nimbiwe kuwa ni msagaji?” Alihoji Maimartha.

Katika kudhihirisha kwamba ni kweli ameamua kumpa kisogo P. Diddy na kujivinjari na bwana huyo, Mai alisema kwamba muda ukifika kila mtu atamjua mpenzi wake, kwani hilo siyo suala la kuficha na mapenzi hayafichiki.

No comments:

Post a Comment