Sunday, March 7, 2010

wanaharakati






Posted by Jide at 1:54 AM 4 comments
3.03.2010
PUNGUA KWA SIKU 7...DIET YA MATUNDA NA MBOGA MBOGA
Kwa watu wanaotaka kupungua kwa muda mfupi kuna diet naifahamu ambayo nita share na nyinyi. Ni ngumu sana siwezi kusema ni rahisi kwahiyo unapoianza uwe umejipanga hasa na kuvumilia. Na ukiharibu hata siku moja inabidi urudi mwanzo uanze upya.
Hakuna cha kwamba ume cheat halafu kanyaga twende unaendelea
Hiyo itakuwa unajiibia mwenyewe...ni ya siku 7 tu na unaweza kuirudia mpaka pale utakapoona umepungua vya kutosha.


Siku ya Kwanza: Asubuhi unakunywa kikombe cha kahawa na kijiko kimoja tu cha sukari
Mchana: Unakula mtunda tu, kula matunda ya aina yoyote kasoro ndizi
Unaruhusiwa kula hata kikapu kizima ukitaka ila jitahidi kula matunda ya rangi mbali mbali na usiku hali kadhalika. kumbuka ndizi haziruhusiwi
Pia hakikisha unakunywa maji kwa wingi sana.

Siku ya pili: Asubuhi ni kikombe cha kahawa na kijiko kimoja cha sukari na kiazi cha kuchemsha
Mchana na usiku ni mboga mboga za aina zote utakazotaka ila jitahidi kuzipika bila mafuta kabisa ukishindwa weka kijiko kimoja tu cha mafuta
Maji kila wakati kwa wingi kuaznia asubuhi hadi unaingia kitandani


Siku ya Tatu: Asubuhi kikombe cha kahawa kama mwanzo, Mchana ni matunda na mboga, hali kadhalika usiku ni matunda na mboga na maji kwa wingi. Matunda ya aina zozote kasoro ndizi


Siku ya Nne: Asubuhi kikombe cha kahawa,..Wali na Mboga mboga mchana, Usiku unakunywa bakuli kubwa la supu ya mboga mboga na maji mengi

Siku ya Tano: Asubuhi kikombe cha kahawa, Kwa muda uliobaki wa mchana hadi usiku unakunywa maziwa Glass 3 zilizojaa vizuri na Ndizi mbivu 8. Usisahau kunywa maji mengi sana


Siku ya Sita: Asubuhi kikombe cha kahawa, mchana na usiku unakula wali na nyanya mbichi. Idadi ya nyanya inatakiwa iwe 6, yaani 3 mchana na 3 usiku. Unaweza kuzikamulia hata ndimu na kuweka chumvi kidogo ukadondoshea na ka kitunguu ikawa kama kachumbari ili isikinaishe mdomoni, manake kula nyanya mbichi napo yataka moyo


Siku ya Saba: Asubuhi kikombe cha kahawa, Mchana na usiku unakula wali na mboga mboga na juice fresh na maji ya kutosha


Kumbuka siku zote unazotakiwa kula wali, pima kisizidi kikombe kimoja na ukiweka mafuta yasizidi kijiko kimoja, usije ukapima mchele vikombe vinne utaua bendi.
Diet haiendi hivyo


Baada ya hapo unaweza kupumzika siku 3 halafu ukarudia tena, ila hizo siku unazopumzika jitahidi kukwepa vyakula vya wanga na mafuta, na ule kiasi kidogo sana cha chakula.
Ukifanikiwa usisite kunijulisha, ukikwama pia utaniambia. Kuna diet ya red snapper tu peke yake na karot huenda hiyo ikawa nafuu ila ni ya siku 13




Posted by Jide at 6:31 AM 39 comments
UNATAKIWA UENDE NA MCHUMBA KWA SONARA UKAJICHAGULIE PETE?? AU UNATAKIWA URIDHIKE NA SUPRISE UTAKAYOLETEWA HATA KAMA NI NDOGO NA SIO YA BEI??





Nimeulizwa swali eti mtu ukiwa unachumbiwa kabla mchumba hajakuvisha pete unatakiwa uende nae dukani kujichagulia au unatakiwa uridhike na yoyote atakayo kuletea.


E-mail niliopokea leo, ni mtu analalamika kuwa pete alioletewa ni mbaya na hajaipenda lakini anajisikia vibaya kumwambia mpezi wake kuwa hakuipenda hiyo pete.
Sababu alizozitoa ni kwamba pete yenyewe ni ndogo sana anaona haina thamani ya kuwekwa kidoleni kwake.
Anasema ni nyembamba sana na inaonekana ni ya bei nafuu.......Labda alitaka kubwa kama ya kwenye picha ya kwanza hapo juu


Lakini kwa mtazamo wangu naona mapenzi sio thamani ya pete, maadam yule aliekupenda kakutunuku na pengine uwezo au taste yake ni hiyo.
Sasa nikaona hivi mtu unatakiwa uende na mwenzio kwa sonara ili ukajichagulie pete ya uchumba au hata ya ndoa unayoitaka wewe au ukubali chochote utakachonunuliwa.
Nitafanya jitihada za kutafuta baadhi ya wasichana waliochumbiwa au hata kuolewa wanipe mitazamo yao na jinsi gani walichukulia walipoona pete zao kwa mara ya kwanza.


Na mimi nitawaambia ya kwangu