Monday, October 11, 2010

pata koti zuri la mvua


ukitaka kujisitiri wewe mcheki huyo cjui mama, binti au nani vile ujipatie koti zuri la mvua

JAMAICA C MCHEZO




Hapa warembo na washikaji kibao wakipita sehemu tofautitofauti wakiponda raha kwenye hii sayari ya tatu

JK,MWANA FA, NA PROF.JAY WATINGA KWENYE BIRTHDAY YA KIKWETE


PROF.JAY NA MWANA FA WAKIPIGA STORY MBILI TATU IKIWA NA KUMPONGEZA JK KUFIKISHA 60YRS.

ABDALLAH RAMADHANI CHANNEL 10-AFARIKI DUNIA


Picha na habari kwa hisani ya Global Publishers
Kituo cha Televisheni cha Channel TEN na Redio ya Magic FM cha jijini Dar es salaam kimepata msiba kwa kuondokewa na mmoja wa watangazaji wake mahiri na vijana, Abdallah Ramadhani (Pichani) ambaye amefariki dunia katika ajali ya gari Ijumaa wiki hii.

Marehemu Abdallah Ramadhani alipata ajali hiyo akiwa njiani mjini Beira, Msumbiji akitoka Afika Kusini kurejea Tanzania Alhamisi tarehe 7 mwezi huu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa marehemu alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Prado ambayo ilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara kadhaa na hivyo kusababisha kifo chake mara baada ya kufikishwa hospitalini.

Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyompasua kichwa, familia yake ilifahamishwa ambapo mdogo wake aitwae Hussein alikwenda kumuangalia hospitali alikolazwa kabla ya kufariki.

Abdallah atakumbukwa na watazamaji wa Channel TEN kwa usomaji wake wa taarifa za habari kwa umakini na ufasaha na kwa wasikilizaji wa Magic FM. Kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa katika mapumziko ambayo aliyatumia kwenda nchini Uingereza kwa siku kadhaa kabla ya kupitia Afrika Kusini ambako alipumzika kwa siku chache na baadaye kuamua kurejea nchini Tanzaniakwa njia ya barabara kupitia Msumbiji.

Pole kwa ndugu, jamaa na nyote mlioguswa na msiba huu.
Apumzike pema Abdallah Ramadhani.

AMEN.